Faustini na Jovita

Bikira Maria na Mtoto Yesu pamoja na Wat. Jovita na Faustino, kazi ya Vincenzo Foppa.

Faustini na Jovita (walifariki Brescia, Lombardia, Italia Kaskazini, 120 au 124) walikuwa Wakristo ambao walifia dini yao chini ya kaisari Hadrian.

Inasemekana Faustini alikuwa shemasi na mwenzake mhubiri waliopigania sana imani.

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 15 Februari[1].

  1. Martyrologium Romanum

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search